Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

00:00
00:00

Episode's summary

Baada ya mkutano wa kimataifa wa tabianchi COP31 kutamatika bila makubaliano mapya ya namna mataifa yanatakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, macho yote sasa yanaelekezwa mkutano ujao COP32. COP31 haikufanikiwa kuwa ya utekelezaji wa ahadi kama ilivyotarajiwa na wengi hasa mataifa yanayoendelea, ikiwemo bara la Afrika ambalo lilikuwa na matumaini ya nchi tajiri kutimiza ahadi zao za ufadhili wa kifedha.

Episodes

269-

Mkutano wa COP31 umehitimishwa bila makubaliano muhimu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Baada ya mkutano wa kimataifa wa tabianchi COP31 kutamatika bila makubaliano mapya ya namna mataifa yanatakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, macho yote sasa yanaelekezwa mkutano ujao COP32. COP31 haikufanikiwa kuwa ya utekelezaji wa ahadi kama ilivyotarajiwa na wengi hasa mataifa yanayoendelea, ikiwemo bara la Afrika ambalo lilikuwa na matumaini ya nchi tajiri kutimiza ahadi zao za ufadhili wa kifedha.

27 Nov 2026
268-

Kenya: Kuchakata Magazeti ili kuunda penseli, mbinu bora ya utunzaji wa mazingira

Nchini Kenya, kundi la wajasiriamali limebuni mbinu ya kipekee ya kubadilisha sekta ya elimu kwa kutumia magazeti ya zamani kutengeneza penseli, huku lengu kuu likiwa kuchangia katika uhifadhi wa mazingira. Kila mwezi, kiwanda hicho cha MOMO pencils kinachakata zaidi ya tani 5 za magazeti yaliyotupwa, na kuunda penseli, hatua inayosaidia kuokoa zaidi ya miti 85 ambayo ingekatwa ili kutengeneza penseli za mbao. Nilizuru kiwnda cha MOMO pencils na kuandaa makala yafuatayo ya mazingira leon dunia yako kesho.

19 Nov 2026
267-

Ajenda ya Nishati Safi na Vitendo Badala ya Maneno Zatawala Mazungumzo ya COP31 Uturuki

Katika mkutano wa tabia nchi mwaka huu COP31, jijini Antalya, Uturuki, wadau mbalimbali wamesisitiza dunia kuondoka katika kutoa ahadi na kuanza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija. Sayari imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa mwaka huu unalenga zaidi kuharakisha mabadiliko ya nishati safi na kusukuma vitendo madhubuti vya kimataifa. Nchi zimesisitiza kuwa muda wa mijadala umekwisha na ni muda sasa wa utekelezaji wa vitendo. Nimefanya uchambuzi na Cherop Soy kutoka shirika la Enzi Ijayo, akizungumzia masuala ya nishati safi kama vile matumizi ya magari ya umeme.

11 Nov 2026
266-

Mkutano wa COP17: Hatua Mpya Zazinduliwa Kuokoa Viumbe Hai Duniani kule Armenia

Wakati ulimwengu ukiwa katika njia panda kutokana na kasi ya kupotea kwa viumbe hai na mabadiliko ya tabianchi, mji mkuu wa Armenia, Yerevan, kuanzia Oktoba 19-30 mwaka huu ulikuwa kitovu cha matumaini mapya. Kupitia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai wa COP17, viongozi wa kimataifa, wanasayansi, na wanaharakati wamekutana sio tu kujadili changamoto zinazokabili sayari yetu, bali kuweka Ahadi ya Yerevan, mpango ambao unalenga kugeuza maneno kuwa vitendo ili kulinda utajiri wa asili wa dunia yetu kwa vizazi vijavyo. Katika makala haya nimezungumza na Stephen Basele, mkurugenzi wa wakfu wa malengo ya wafugaji, kaskazini mwa Kenya aliyehudhuria mkutano huu kutetea haki za jamii asilia.

11 Nov 2026
265-

Awamu ya pili: Kongamano la masoko ya kaboni barani Afrika, Kigali

Pamoja na Bwana Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, tunaendelea na awamu ya pili ambapo nilikuahidi kuangazia ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha kuwa biashara ya kaboni zinawakilisha upunguzaji halisi wa gesi chafuzi.

26 Oct 2026